Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo ameachia Remix ya wimbo wake Bia Tam na kuuita Yanga Tam ikiwa ni wimbo maalum kwa klabu ya mpira wa miguu ya Yanga.
Marioo ametambulisha wimbo huo mbele ya waandishi wa habari pamoja na msemaji wa Yanga, Haji Manara leo jijini Dar es Salaam.
Marioo amesema kuwa sasa ameamua kuamia Yanga baada ya kuachana na Simba hivyo ameamua kutunga wimbo kuhusu klabu yake hiyo mpya.
“Sasa nipo rasmi Yanga, zamani nilikuwa nashabikia timu ile nyingine. Mimi sipendi stress, tu-enjoy na wimbo huu wa Yanga Tamu“. Amesema Marioo
Wimbo huo umeachiwa leo rasmi katika platforms mbali mbali za kupatikana kwa wimbo huo hivyo mashabiki wa Yanga wanatakiwa kuutafuta wimbo hhuo.