Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa yupo kwenye mahusiano mapya na ayupo single kama baadhi ya watu wanavyohisi.
Diamond Platnumz alikiri kwamba mahusiano yake mapya yamejawa na mahaba mazito na yanampa raha kubwa kwasasa.
“Kwasasa nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na nampenda sana mpenzi wangu hivyo watu wajue sipo single nipo kwenye mahusiano” Alisema Diamond
Mwanamuziki huyo hata hivyo hakufichua jina wala chochote kuhusu mpenzi wake wa sasa licha ya kuthibitisha kuwa yupo kwenye mahusiano.
Aliweka wazi kuwa anampenda sana malkia anayechumbia kwa sasa huku akidhihirisha kuwa anayathamini mahusiano yao.
Miwanamuziki huyo alikuwa kwenye mahusiano na wasanii tofauti tofauti kama vile Hamisa Mobetto na Wema Sepetu kutoka Tanzania, Zari Hassan kutoka Uganda na Tanasha Donna kutoka Kenya.