Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu amewashukuru wote walioudhulia katika Usiku wa Mahaba Ndi Ndi Ndi katika ukumbi wa Mlimani City siku ya Jumatatu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram mwanamuziki huyo amewashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wake waliojitokeza kwenye onesho hilo.
Zuchua ameandika “Naomba nitangulize shukrani kwa waalikwa Na wahudhuriaji wote mliojitokeza jana kwa wingi wa kishindo Kwenye Usiku wa Mahaba Ndi Ndi Ndi.
Pia ameandika kuwa “Niseme kidhati kabisa nimefarijika na nafurahi napokea Positive comments kuhusu show ya jana inanifariji mimi na kamati yangu nzima ya maandalizi tunawashukuru sana Tickets ziliisha .Meza zilijaa ukumbi ulifurika .Hakika shughuli bila nyinyi haiwi nasema asante kwenu”.
Mwisho ameamaliza kwa kuandika “Naomba nichukue nafasi hii kutoa shukrani kwa Viongozi wetu wakiongozwa na Mh Nape kwa kuacha kazi zenu na kuja kufurahi nasi. Nashukuru Media na wadau wote wa burudani kwa kua nasi bega kwa bega .Niombe pia msamaha kama kutakua na makosa kadhaa yaliyojitokeza . Mashabiki zangu wapenzi wangu Bila ya nyinyi mimi si zuchu nawapenda sana Asante sana
Onesho hilo lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na mashabiki na baadhi ya wadau wa muziki wa Bongo Fleva nchini.