Siku iliyokuwa inasubiliwa kwa hamu na wapenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu iliyokuwa inafahamika kama ‘Mahaba Ndi Ndi Ndi’ imehitimishwa jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mahaba Ndi Ndi Ndi ni siku maalam ya Valentine Day ambayo iliandaliwa na lebo ya WCB iliyokuwa chini ya mwanamuziki nyota Tanzania, Diamond Platnumz.

Viongozi wa Serikali na watu maarufu walihudhuria onesho hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria hafla hiyo ni waziri wa Habari, Nape Nnauye, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohamed Mchengerwa na wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es Salaam.

Kwenye siku hiyo Zuchu ameingia ukumbini hapo akiwa na Diamond Platnumz huku akiwa amevalia gauni la rangi nyeupe na Diamond akivalia suti nyekundu.

Wasanii mbali mbali walitoa burudani kwenye onesho akiwamo, Bushoke, Cassim Mganga, Mac Voice, Khadija Kopa, Patricia Hilary pamoja na Zuchu mwenyewe.

Tofauti na matarajio ya wengi ambao walidhani kuwa Diamond Platnumz anaenda kumvisha pete Zuchu lakini halikutokea tukio hilo mpaka mwisho wa hafla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *