Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jux amefunguka ukweli wa kilichotokea kati yake na Harmonize baada ya kutangazwa kwake kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Afro East Carnival.
Jux ameweka wazi kuwa kitendo hicho amekitafsiri kama utovu wa nidhamu kwa madai ya kuwa Harmonize amemkosea heshima.
Nikamwambia mpe namba ya Ray ambaye ni meneja wangu, ukapita muda kidogo, sasa leo naamka nikatumiwa artwork na timu yangu wananiuliza kama hii show nimekubaliana nayo, Nikawaambia hapana, Na hata hata Ray alisema pia hakupigiwa simu.
Lakini pia Ray aliwapigia simu akaongea nao, wakamwambia kuna wasanii ambao Harmonize anaongea nao mwenyewe, akasema anadhani Harmonize atakuwa amekubaliana nao ndio maana artwork ikatengenezwa, nikawaomba waishushe lakini walikataa.
Nikamcheki Harmonize nikamuuliza kama aliongea na timu yangu akasema aliongea nayo, ila ngoja awacheki tena, mimi nikamwandikia hakuna makubaliano yoyote na ulitakiwa uhakikishe kama ambavyo ulinicheki mara ya kwanza, kwangu naona kama unanichukulia poa na dharau.
Hiyo message haikujibiwa na muda unazidi kwenda ndio nikaenda pale nika-comment.” alisema Jux. Jux ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano maalum aliyofanya kupitia kipindi cha Empire.