Familia ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joseph Haule imekubali achangiwe fedha za matibabu.

Profesa Jay alipokelewa hospitalini hapo wiki ya pili ya mwezi Januari na kueleza kuwa alikuwa katika chumba cha uangalizi maalumu wa wagonjwa (ICU) akiendele na matibabu.

Katika mitandao ya kijamii limesambaa tangazo likiomba kuchangia matibabu ya msanii huyo na mkewe wake Profesa Jay, Grace Mgonjo amethibitisha kuwa wameruhusu michango hiyo huku akieleza kuwa kwa wiki moja wanatumia mpaka Sh4 milioni katika matibabu yake hivyo wameona watoe nafasi kwa watu wake kumchangia matibabu.

Tangazo hilo linasomeka “Jinsi ya kuchangia matibabu ya Professor Jay. Michango yote itapokelewa na familia kwa niaba yake kupitia namba 0757 919 192 jina Joseph Haulena namba 07715 919192 jina pia Joseph Haule.

Au kupitia benki huku ikitaja namba ya akaunti kuwa ni 0112044845200.

Tayari wasanii na mastaa mbalimbali wameweka tangazo hilo kama njia ya kuunga mkono kupatikana kwa mchango huo akiwemo Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, AY, mbunifu mitindo Martin Kadinda, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Darasa, Aunt Ezekiel na mfanyabiashara maarufuu Director Joan.

Profesa Jay katika sanaa yake amewahi kutesa na vibao mbalimbali ikiwemo Ndio Mzee, ‘Zali la Mentali, Jina Langu, Nikusaidiaje, Kama Ipo, Kipi Sijasikia na nyingine nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *