Wasanii wa Bongo Fleva, Fid Q, AY na Chege wamefika katika ofisi za Taasisi ya Hakimiliki (COSOTA) kuwasilisha taarifa zao za kibenki na kukamilisha taratibu za msingi ili kuweza kukamilisha zoezi la ulipwaji wa mirabaha yao.

Pamoja na hayo Wasanii hao wamemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuweka msisitizo katika kusimamiwa kwa Hakimiliki za Wasanii pamoja na kuhakikisha wasanii hao wanapata mgao wa mirabaha kwa kazi zao zinazotumika katika maeneo mbalimbali ya biashara.

Halikadhalika wameipongeza COSOTA kwa kuwalipa mirabaha kwani ni muda mrefu hawajapata mirabaha na pia hawajawahi kupata gawio kubwa kama ilivyo katika mgao huo wa sasa.

Kwa mujibu wa sheria wasanii wanaolipwa mirabaha ni wale ambao wamejisajili Cosota kazi zao na pia kazi hizo zimethibitika kuzumiwa kibiashara (economic use) kama vile muziki kupigwa katika vituo vya redio au kazi yoyote ya fasihi mfano kitabi kuingizwa katika matumizi ya kuigizwa katika filamu ya kibiashara.

Iwapo kazi ya msanii haijatumiwa kibiashara hata kama ameiuza na iko sokoni kwa wingi basi hana haki ya mrabaha na wingi wa kutumika kazi ya mtu ndio unaotofautisha ukubwa wa mapato kati ya mtu mmoja hadi mwingine,” amefafanua Ofisa wa Cosota.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *