Serikali ya Tanzania Kupitia COSOTA imeanza kugawa rasmi Mirabaha kwa Wasanii wa Muziki hapa nchini, ikiwa ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan la kutaka wasanii wanufaike na kazi zao.

Na Usiku wa Kuamkia Januari 29 Wasanii mbalimbali wamepokea mgao huo unaotokana na kazi zao kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Redio na Televisheni ambapo Kwaya ya Mtakatifu Cesilia ya Jijini Arusha imeongoza na kuibuka na kitita cha Tsh Milioni 8.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameshika nafasi ga pili kwa kupata mgao wa Shilingi Milioni 7.5, huku akiwa wa kwanza (Namba.1) kwa wasanii wa muziki wa Bongofleva. Wasanii wengine waliopata mgao huo ni pamoja na Rose Muhando, Ambwene Yesaya (AY) Faustina Charles (Nandy), Mauwa Sama, Martha Mwaipaja, Christina Shusho na wengine.

Baada ya kupewa pesa hiyo, Kiba amesema; “20 years in the game, jana nimepata mrabaha wa kwanza, imechukua muda lakini mwanzo mzuri. Sheria ya hakimiliki imeanza kufanya kazi. Asante Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji huu wa sheria. Wizara ya Sanaa na Utamaduni, COSOTA kwa kufanikisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *