Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Dogo Janja amefunguka kuwa hisia za kimapenzi alizonazo kwa mpenzi wake wa sasa Queen Linah ni kutokana na kukamatika kwake na ndiye mwanamke wa maisha yake.
Dogo Janja amesema kuwa, upendo alionao kwa mpenzi wake huyo haulezeki kwani kuna muda anatamani hata awapigie simu maeksi wake awaambie jinsi alivyo na furaha.
“Nashindwa niongee nini, lakini ni ukweli usiopingika kwamba sasa hivi nimekamatika, tena nimekamatika haswaa, huyu mwanamke ananipa kila ninachokitaka.
Pia amesema kuwa heshima, mapenzi ya dhati na vitu vingine vingi ambavyo sisi wanaume huwa tunavipenda kutoka kwa wapenzi wetu, kiasi kwamba najuta kwa nini sikumjua mapema,”.