Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amekanusha kuachana na mpenzi licha ya hapo awali kutangaza kuwa ameachana na mpenzi wake huyo.
Harmonize aliandika ujumbe mbalimbali kupitia instagram stori yake kuwa amerudi tena kwenye maisha ya ubachela baada ya kuumizwa kimapenzi.
Harmonize hakuishia hapo alimu-unfollow hadi mpenzi wake Briana jambo ambalo lilifanya watu waamini kuwa penzi lake na mrembo huyo kutoka nchini Australia limefika ukingoni.
Harmonize amebadili maamuzi kaona bora arudi nyumba aliyoizoea kwani kunguni wake ameshawajua kuliko kwenda kuanza upya. Harmonize ametumia ukurasa wake wa Instagram (Instastory) kwa kuandika kuwa
“Sipo Single tuheshimiane“.
Harmonize hakuishia hapo bali amemfollow tena mpenzi wake huyo na hata kwa upande wa Briana ame-mfollow back Harmonize.