Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Q Chief amewashangaa mashabiki wake kumjia juu baada ya kuonesha maisha yake halisi katika mitadano ya kijamii.
Q Chief au Q Chilla ameonesha maisha yake ya uhalisia kwenye mitandao ya kijamii haswa Instagram ambapo mara nyingi amekuwa akipost video akiwa anapika vyakula vya kiswahili kwenye mazingira ya uswahilini jambo ambalo limefanya mashabiki wahisi kuwa amefulia.
Q Chief amesema kuwa “Mimi sipendi kupikiwa kama chakula chako hakina ladha. Naweza kuwa na 2000 nikapika chakula kikakidhi kila mtu kwasababu ya mazingira. Kwenye ukurasa wangu nikipost picha inakuwa kawaida ila nikipost mtokoto inaenda dunia nzima. Kuna watu wananitafuta wameona biashara baada ya mimi kuanza kupost hivyo vyakula japo nilianza kufanya hivyo kufurahisha watu”
“Hayo ndio maisha yangu, mimi sikutoka jana. Nimepitia adha zote hakuna aibu yeyote mpya kwenye maisha yangu. Haya ni maisha ambayo nataka niyakumbuke kabla sijakufa, maneno hayamsumbui mtu bali yanakujenga“.
Chilla hakuishia hapo amezungumzia pia juu ya msanii Harmonize ambaye amekuwa akiiga upishi wake na kupost Instastory. “Ninachokifanya watu wengine wanaiga lakini wengine wanaona upuuzi ni maisha ya kawaida haitakiwi kuwachanganya”
Kwa upande mwingine Q Chief amefunguka kuhusu ujumbe wake ambao ameuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao wengi wameutafsiri kama kujitabiria kifo au kukata tamaa na maisha
Lakini pia amesema wavuvi wamekuwa watu wema sana kwake pindi anapokwenda kuchukua sama baharini “Wananipenda sana, wanashangaa. Nakaa nao tunapiga stori napata mawazo ya nyimbo mpya, wengine wananiletea samaki“.