Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa aumizwi kichwa na baadhi ya mashabiki wake wanaomkejeli katika mitandao ya kijamii.

Baada ya kuchoshwa na komenti hasi za baadhi ya wafuasi wame, ameamua kuwatolea uvivu akiwaambia wanapaswa wamuache na maisha yake.

Kwa mujibu wa Wema, ujumbe wake uwaendee wale wote ambao wamekuwa wakimkosoa na kumkejeli.

“Yaani binadamu bwana, usipofanya wanasema, ukifanya pia wanasema….sasa sijui hata nifanye nn…Hebu mniache…” Anasema Wema.

Ni wazi kwamba, Wema alikuwa mpenzi wa Diamond; mapenzi yao yalitamaniwa na wengi, lakini hawakuweza kudumu. Miezi michache iliyopita, Wema alikiri kwamba yupo singo, lakini anaweza kumpenda mtu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *