Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny, Fahyma amesema kuwa, anajijua yeye ni mrembo mno, lakini suala la kuachana au kuachwa na mwanaume ni la kila mtu hivyo watu waache kuropoka.
Mwanamitindo huyo anasema kuwa, kuna watu wengi huwa wanakomenti mambo ambayo hayana maana kwenye picha zake, wakijua watamuumiza, lakini wapi.
Anasema kuwa, mara utasikia mtu akisema kama ni mrembo kwa nini ameachwa, lakini anachojua ni kwamba kama mapenzi yakifika mwisho watu huachana tu na hata wawe wazuri kama malaika.
“Binafsi najijua kuwa ni mzuri, tena sana, sasa nawashangaa hao ambao huwa wanakuja kwenye akaunti yangu kunitukana kuwa kama mimi ni mrembo, kwa nini sipo na baba wa mtoto wangu, wanasahau kuwa kuna muda mapenzi huwa yanaisha na yakiisha lazima kila mtu aendelee na maisha yake
Mtu hata uwe mzuri kama malaika, kama upendo haupo tena ni haupo tu,” anasema Fahyma ambaye ni baby mama wa msanii Rayvanny.