Mugizaji wa Bongo Movies, Kajala Masanja ameasema kuwa ameipisha kidogo mitandao ya kijamii ili watu waendelee na shughuli zao maana kila siku akifikiria mambo ya mitandao, yanampotezea muda wake mwingi.
Kajala anasema kuwa,kuna wakati mtu anakubali tu kuandamwa na mitandao ya kijamii, akiamini kuna muda watanyamaza na mtu utaendelea na mambo yako vizuri kama ilivyokuwa mimi kwangu huko nyuma nilivyoandamwa na mtoto wangu (Paula).
“Kwa sasa nimeipisha mitandao kwanza iendelee na kazi zake nyingine, maana kila kukicha ilikuwa ni mimi, lakini mwisho wa siku nilikubali tu kila kitu nikaa kimya na mwisho wa siku walitusema na wakamaliza yote, wakatulia tuli,” anasema Kajala.
Muigizaji huyo ameamua kupisha mitandao kutokana na kuongelewa vibaya yeye pamoja na mtoto wake Paula Kajala kutokana na aina ya maisha wanayoishi.