Uongozi wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide inayomilikuwa na Harmonize umetangaza kuacha kufanya kazi Rapa Country Boy January 08, 2022.

Uongozi huo umetoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wao rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo wameainisha kuwa kuacha kufanya kazi na staa huyo kunatokana na kumalizika kwa mkataba kati yao

Konde Gang wameandika “TAARIFA: Mkataba Kati Ya Konde Music Worldwide Na Country.

Kuanzia Leo Country Wizzy Atakuwa Msanii Anaejitegemea Baada Ya Kufikia Makubaliano Ya Pande Zote Mbili. Konde Music Worldwide Inamtakia Kila Lenye Kheri Country Wizzy Kwenye Career Yake Ya Music Pamoja Na Maisha Kwa Ujumla

All the Best Wizzy!!”

Conutry Boy alitangazwa kuanza kufanya kazi na uongozi wa lebo hiyo ya Konde Music Worldwide mnamo September 2020.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *