Chama Cha Wasanii wa Kizazi Kipya ‘TUMA’ walifanya uchaguzi wa nafasi nane chini ya usimamizi wa viongozi wa BASATA na Shirikisho la Muziki ambalo liliwakilishwa na Rais wake Ado November pamoja na Katibu Mkuu wake, Rapa Fid Q.

Uchaguzi huo uliisha salama kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi ambazo walijiwekea wasanii wao na washindi katika nafasi nane kutangazwa na matokeo kukubalika.

Soggy Doggy alishinda nafasi ya Ukatibu Mkuu, huku Mike Tee ambaye alikuwa anagombea Uenyekiti kuangukia pua baada ya kugaragazwa na Briton.

Witness alishinda Uwenyekiti Msaidizi bila kupigwa huku BagDady na yeye akishinda nafasi ya na kutangazwa.

Baada ya zoezi zima la Uchaguzi kumalizika, aliinuka BagDad na kusema kwamba hawawezi kufanya kazi na Briton ambaye ameshida nafasi ya Uenyekiti na kumbwaga Mike Tee kwa kura nne kwa madai ameshindwa kuendeleza TUMA kwa miaka iliyopita hivyo wanaomba aondolewe au tao wajihudhuru nafasi zao.

Orodha ya washindi ambao walitangazwa.

1. Mwenyekiti – Braton

2. Makamu Mwenyekiti Witness

3. Katibu Mkuu – Soggy

4. Katibu Mkuu Msaidizi – Baghdad

5. Mweka hazina – Azma Mponda

6. Mweka hazina msaidizi – Dan Laizer

7. Afisa Uhusiano na Ukuzaji muziki – Kwame

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *