Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amesema kuwa anamshukuru Mwenyezi Mungu amempumzisha salama mama yake kipenzi nyumbani kwa wazazi wa mama yake huyo, lakini mambo mengine ya nyumba anawaachia waja.

Lulu Diva amesema kuwa, kikubwa alichofanikiwa kama mtoto wa Kiislam ni kumpumzisha mama yake sehemu salama na nyumbani kwao anakostahili na kumuombea ipasavyo, lakini mambo mengine anawaachia watu wa mitandao wanaoweza kuzungumza kila jambo bila kuchuja.

“Unajua walimwengu wana utofauti sana, ukimuona mtu anaongea, tena anaongea kwenye wakati mgumu ambao mtu anapita wa kuondokewa na mama yake mzazi’.Alisema Lulu Diva

Pia amesema kuwa unamkuta mtu anazungumzia mambo ya nyumba bila hata kujua chochote, ni kuachana naye maana kwangu kikubwa nimempumzisha mama yangu salama,” anasema Lulu Diva ambaye alikuwa mtoto wa pekee kwa mama yake.

Hivi karibuni Lulu Diva alifiwa na mama yake na kwenda kupumzishwa kijijini kwao, Muheza jijini Tanga ambapo huko ndiko ukaibuka mjadala kwamba, nyumba ilikuwa haifanani na ustaa wa mrembo huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *