Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbosso amefunguka na kusema kuwa yeye ni miongoni wa wasanii nyimbo zao zimepotea katika studio ya Mocco Genius.
Mbosso ameguswa kwa kwa kupoteza demo 54 za muziki wake kwenye upotevu wa kazi mbalimbali za wasanii zipatazo 500 alizohusika kuziandaa mtayarishaji Mocco Genius tangu mwaka 2019 mpaka sasa.
Mtayarishaji huyo ambaye pia ni msanii wa muziki ameelezea kuwa kifaa kilichokuwa na kazi hizo kimepata hitilafu na amekuwa katika hatua za kuhakikisha anarejesha kazi hizo kwa muda mwezi sasa bila mafabikio.
Mbali na Mbosso wasanii wengine wakioguswa na tatizo hilo ni mwimbaji Malkia Karen aliyeweka ujumbe wake akigusia album isibainike kama aliandaa album kwa Mocco Genius ambayo nayo ni miongoni mwa kazi zilizopotea.