Aliyekuwa mpenzi wa msanii Rayvanny aitwae Fahyma inaaminika kuna vitu havijakaa sawa kwa upande wake kwani miezi miwili iliyopita alisema kwamba, mwaka huu wa 2021 usingemalizika bila kuolewa, lakini siku zinazidi kuyoyoma na hakuna hata dalili ya kuolewa.
Sasa, wakati mashabiki wa Fahyma ambaye ni mwanamitindo wakitafakari hilo la kuolewa, ameibuka na lingine akidai kwamba, mwaka ujao wa 2022 anatarajia kuzaa mapacha.
Ishu hiyo imeibua gumzo kama lote kwani kuna wanaoamini amerudiana na Rayvanny baada ya mpenzi wa jamaa huyo ambaye ni Paula Kajala kwenda masomoni nchini Uturuki.
Wengine wanajiuliza kama siyo Rayvanny ni mwanaume gani huyo ambaye Fahyma anatarajia kupata naye watoto mapacha?