Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia ukurasa wao rasmi wa instagram, Tanzania National Park wamemkaribisha Rapa wa nchini Marekani Rick Ross.
Rick Ross alikatibishwa kwa ishara ya kutembea mlima Kilimanjaro na mbuga ya wanyama ya Serengeti, kwa kupandisha picha ya msanii huyo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Baada ya post hiyo Rapa Rick Ross aliitupia picha hiyo kwenye Insta Story yake na kuwashukuru waliofika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kupiga picha wakiwa wameshikilia picha yake na kumkaribisha kutembelea Mlima huo.
Mwanamuziki huyo uhenda akatua nchini Tanzania kutokana na ukaribu wake na mwanamuziki na mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobeto ambaye walikuwa wote nchini Dubai.