Muigiaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya amesema kuwa, kutokana na kujua kulihimili jiko vizuri ni ngumu hata anapopata mpenzi akaingia kwenye anga zake, basi hawezi kuchomoka kirahisi.
Irene amesema kuwa mwanaume hawezi kumuacha kwasababu habari yake anaijua na mwanaume siku zote ni kula chakula kizuri na mengine ni mbwembwe tu.
Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume anasema kuwa, kitu kinachomlinda na kumuonesha yeye ni mwanamke sahihi ni kwenye upande wa jikoni kwa sabau harembi na anajua kusimama kama mwanamke anayelijua jiko alitumiaje.
“Huu mkono wangu ni hatari sana kwenye mapishi na ninakuambia ukiingia kwenye anga zangu huchomoki.
Sehemu yangu ninayojidai ndiyo hii, nikikupa pishi langu kubanduka kwenye himaya yangu ni ngumu sana, lakini kitu kingine sifa kubwa ya mwanamke jiko,” anasema Uwoya huku akila nyama ambayo ameichoma nyumbani
kwake.