Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa, maisha yana siri kubwa hivyo yanahitaji uvumilivu mkubwa tofaui na hivyo unaweza kugombana na kila mtu kwenye ulimwengu huu.
Wema anasema kuwa, kuna mtu anaona wazi anamchokonoa na kumkera kupitia mitandao ya kijamii, lakini ukweli ni kwamba silaha kubwa ni uvumilivu na kunyamaza.
“Hakuna kitu kizuri kama kubeba uvumilivu kwenye moyo wako maana maisha yana siri kubwa mno na kufanya hivyo utaepusha mambo mengi.
Pia amesema kuwa ndiyo maana watu siku hizi wanashangazwa na uvumilivu ambao niko nao kwa sasa na unazidi kunijenga,” anasema Wema ambaye kwa hivi sasa amepoa, tofauti na zamani.