Aliyeekuwa mke wa staa wa RnB Bongo, Ben Pol, Anerlisa amemtuhumu Ben Pol kwa kutoheshimu ndoa yao miezi michache baada ya wawili hao kuachana.

Anerlisa ambaye wikiendi iliyopita alitua Dar kwa shughuli zake binafsi anasema aliumia baada ya Ben Pol kufunguka mambo mazito hadharani kuhusu ndoa yao.

Anasema chochote alichokuwa akikifanya Ben Pol kilikuwa kinakwenda kinyume na kile walichofundishwa baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha.

Anerlisa anafichua kwamba, Ben Pol alibadili dini na kuwa Muislam kabla ya kurejea Ukristo baada ya wiki mbili. Anerlisa anasema hatajutia kuchumbiana wala kuachana na Ben Pol kwa sababu anaamini kila kitu ni funzo.

Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa ya kifahari na kudumu takriban miaka miwili kabla ya kuachana kwa kile kilichosemekana kwamba ni usaliti. Hata hivyo, walikuwa bado hawajajaaliwa mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *