Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ameingia kwenye rekodi nyingine ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuingiza wimbo kwenye chati za mtandao maarufu wa Billboard.
Rayvanny ambaye pia ni mkurugenzi wa lebo ya Next Level Music ‘NLM’ anaingia kwenye rekodi hii mpya na wimbo ‘Mama Tetema’ aliomshirikisha Maluma kutokea Colombia uliotoka rasmi wiki mbili zilizopita.
Rayvanny anashika rekodi hii kwenye tasnia ya muziki Tanzania baada ya kuwa Msanii wa kwanza Afrika kutoa Burudani kwenye jukwaa la utoaji wa tuzo za MTV Ema.
Aidha, itakumbukwa kuwa Rayvanny ndiye msanii wa kwanza anayeshikilia rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo ya BET nchini Tanzania.