Mwanamuziki wa Bongo Fleva, 20 Percent amefunguka na kusema kuwa yupo mbioni kufanya kolabo na mwanamuziki mwenzake Harmonize ambayo karibia inakamilika.
20 Percent ambaye alitamba sana enzi hizo anasema kuwa atafanya wimbo mpya na Harmonize ila hawezi kukubali wimbo wake wowote kurudiwa.
Hakuishia hapo 20 Percent amemtolea mfano Saida Karoli ambaye wimbo wake ulirudiwa na Diamond na Rayvanny na kusema kuwa hakunufanika na kolabo hiyo.
20 Percent ameongeza kuwa kufanya kazi na Harmonize haimaanishi kuwa atakuwa chawa wa Harmonize na wala hataki kujifunga na upande wowote.