Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amekiri kwamba hali ni mbaya na amezidiwa na mwili wake hivyo sasa anarejea gym kwa ajili ya kurejesha muonekano wake wa awali.
Shilole ameweka picha yake ya zamani iliyomuonesha akiwa mwembamba na kuandia;“Je, umemjua huyo binti hapo? Kama ndiyo basi kakubali kurudi gym na anataka traina wa kumfuata kwake, malipo siyo shida.
“Kikubwa mazoezi yawe standad siyo kokomoana maana walimu wengine khaaaaa!”Shilole amekuwa akisemwa vibaya na kupewa majina mbalimbali kama kibanda cha simu kutokana na kuwa na mwili mkubwa.
Mwanamuziki huyo kwasasa ameamua kuanza mazoezi kwa ajili ya kupunguza unene ili aweze kurudisha mwili wa awali ambapo alikuwa na mwili mdogo sana.