Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Lulu Diva amesema kuwa suala la kukosa mtoto linamtesa na kwamba anamuomba Mungu amjalie uzao wake na yeye.

Lulu Diva amesema kuwa, kwa sasa hana mtoto ila anatamani mno siku moja aitwe mama kama walivyo wamama wengine kwani huko ndiko kuwa mwanamke kamili.

“Kwa sasa sina mtoto hata wa dawa ila kiukweli natamani sana kuitwa na mimi mama Mungu anijaalie juu ya hilo,” anasema Lulu Diva ambaye amekuwa akimficha mpenzi wake.

Lulu Diva kwasasa anafanya vizuri kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva kutokana na nyimbo zake kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki Bongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *