Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ndiye msanii wa pili kwa idadi kubwa ya watazamaji wa jumla katika Mtandao wa YouTube Afrika Mashariki akiwapoteza kabisa wenzake wakubwa kama Harmonize na Alikiba.
Rayvanny aliyejiunga na mtandao huo Machi 17, 2016 anachukua nafasi hiyo ya pili akiwa na jumla ya views zaidi ya million 643.8 baada ya kumpita Harmonize ambaye alijiunga mwaka mmoja nyuma yake na sasa ana jumla ya views milioni 643.7.
Diamond Platnumz ndiye kinara wa jumla wa views kwa nchi zinazopatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika akiwa na jumla ya watazamaji zaidi ya bilioni 1.5.
Rayvanny ambaye kwasasa ana miliki lebo ya Next Level amekuwa anafanya vizuri kwenye muziki toka ajiunge na lebo ya WCB.