Mwanamuziki wa nyimbo za Asili, Mrisho Mpoto aisimamisha Wilaya ya Bagamoyo kwa saa moja kwa ajili ya kutoa burudani kwenye Tamasha hilo.

Hivyo ndivyo unaweza kusema baada ya msanii huyo kutoa burudani ya aina yake katika tamasha la sanaa na utamaduni Bagamoyo.

Mpoto aliyepanda jukwaani na wasanii wake saa 5:11 alishuka saa 6:11  na kutoa  burudani ya bandika bandua.

Burudani hizo ni pamoja na kuimba, kucheza, ngoma, sarakasi, kuchezea moto na kuchezea nyoka jambo walilolifanya kwa saa nzima huku watu wakiwa wametulia kuwafuatilia.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwananchi Digital akiwemo Naima Mwinyi, amesema Mpoto ni mtumbuizaji kwani ni msanii ambaye huchoki kumwangalia anachokifanya jukwaani kuwataka wengine kujifunza kutoka kwake.

Ukiachilia mbali Mpoto, wengine waliofunika ni Rapcha na Barnaba ambaye hata alipokuwa akiaga kushuka jukwaani watu walikuwa wakipiga kelele kumtaka aendelee.

Barnaba aliwambisha watu nyimbo zake ikiwemo Cheketua, Washa, Loverboy, Tuachane mdogomdogo na nyingine.

Wakati Rapcha yeye alipanda na Lissa wake jukwaani huku akiwa anasukumwa katika kiti cha mgonjwa akiwa na majeraha kama ilivyokuwa kwenye video ya wimbo wake wa ‘Lisa’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *