Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jux amefunguka na kusema kuwa, biashara yake ya mavazi African Boy ilianza kwa mtaji wa shilingi 400,000 na ni kipindi ambacho alikuwa anasoma nchini China.

Jux anauza tisheti, kofia, viatu, mabegi, makava ya simu na bidhaa nyingine zenye brandi ya African Boy.

Jux anasema Aprili 12, 2018 alisaini makubaliano na kampuni ya Vendome kutoka China kwa ajili ya kutengeneza bidhaa hizo za ya African Boy, wakati huo akisoma nchini humo katika Chuo Kikuu cha Guangdong kilichopo Guangzhou.

“Nilianza na pisi 50 za kofia, nilipozileta hapa siku hiyo hiyo zikaisha, nikaongeza tena, nikaona mbona hii biashara imechagamka, japo nilikuwa sina pesa nyingi za mtaji, nikawa naenda hivyo taratibu.

“Baada ya kipindi kifupi niliweza kuukuza mtaji hadi kufikia kati ya Dola za Kimarekani 2,000 na dola 3,000 sawa na shilingi milioni 4.6 na milioni 6.9.

“Hizo pisi 50 kila moja nilikuwa nanunua kwa shilingi 8,000 sasa hapo gawanya shilingi 400,000, ilikuwa ni pesa ndogo sana. Sasa ikaja kila wiki ikawa naongeza, hadi kufikia mwezi nilikuwa nimeshaweza kufikisha dola 2,000 hadi 3,000,” anasema Jux.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *