Meneja wa Diamond Platnumz, Babtu Tale atamani wasanii waliounda kundi la Yamoto Band kufanya tamasha maalum la kumshukuru Mkubwa Fella kutokana na mchango wake kwao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale amendika “MKUBWA FELA ANASTAHILI SANAMU YA HESHIMA. Usiku wa jana sijalala kabisa, kwani nilizongwa na kumbukumbu ya safari ya Muziki na maisha.
Mbali ya kuwakumbuka watu wengi, Kichwani mwangu ilikuja picha ya darasa lenye Watoto Wanne wenye Masauti yanayogonganisha mashairi yasiyochosha.
Ni kweli nilikuwa nikiliwaza darasa lenye historia kubwa nalo ni “YAMOTO BAND”.
Ni miaka mingi imepita toka kundi hili lililowahi kuwa na mvuto mkubwa livunjike.
Na leo sijawaza juu ya kwanini limevunjika!?..Bali nimewaza na kutafakari Uthubutu, Malengo, Kujitoa na Uwekezaji uliofanywa na Mkubwa Fella.
Ndio wakiandaa onyesho hili itakuwa wameenzi mchango wake Kwa vitendo, na nayaongea haya kwa pumzi hii niliyojaaliwa leo.
Natamani kuona JUKWAA MOJA, HESHIMA KWA FELA TUKIWA HAI.
Najua naweza kukwaza hisia na matakwa ya Wahusika, lakini MKUBWA FELA ni Mtu muhimu kwakuwa aliwafungulia milango ya Mjini na Muziki.
Natamani MKUBWA FELA ajengewe SANAMU pale Temeke,…kwakuwa kukuza kipaji kimoja kunahitaji miaka zaidi ya mitano, lakini MKUBWA FELA alikuza vipaji vinne kwa muda mfupi. Mzee wa jua la utosi zingatia hili Chambuso.