Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny aitwae Fahyma amefunguka na kusema kuwa amchukii Paula licha kuwa penzini na Rayvanny.

Fahyma ambaye ni mwanamitindo na mbunifu wa mavazi maarufu Bongo amefunguka juu ya mambo mengi ikiwemo ishu ya kurudiana na Rayvanny wakati huu ambao Paula yupo masomoni nchini Uturuki.

Fahyma amesema kuwa, anaheshimu na kumpenda Rayvanny ambaye ni staa wa Bongo Fleva kwani ni baba wa mtoto wake na wanashirikiana kmlea mtoto huyo, lakini haitatokea wakarudiana tena au wakawa kwenye mapenzi.

Fahyma anasema kuwa, mwanawe Jaydany anaishi kishua kwa sababu anapata kila kitu kutoka kwa baba yake, Rayvanny.

Kuhusu Rayvanny kudai kwamba amemmisi Paula na kumuita mke, Fahyma anasema kuwa ni haki yake kabisa kwa sababu ni watu ambao wanapendana.

Kuhusu mwanawe kwenda kulelewa na Paula, Fahyma anasema anaweza akamchukua kisha akamrudisha kwake, lakini si kumuachia kabisa ili amlee.

“Simchukii Paula na wala siwezi kumchukia…” Anasema Fahyma.

Kabla ya kutengana mwaka jana, Fahyma na Rayvanny walidumu kwenye mapenzi kwa miaka saba na kujaaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydany kabla ya jamaa huyo kunyakuliwa na Paula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *