Mwanamuziki Hip Hop Bongo, Rosa Ree amesema kuwa wanaume wasiogope kuwa na vitambi kwa kuhofia kuachwa na wake zao, badala yake wajikite zaidi kwenye kutafuta mkwanja tu; hapo kila kitu kitakwenda sawa, sawia.

Rapa huyo namba moja Bongo anasema kuwa, anashangaa kuona kuna wanaume bado wanahangaika kupunguza miili yao hasa vitambi, halafu wanasahau kutafuta pesa, mwisho wake ndiyo wanakuja kuitwa ‘vibenteni’, jambo ambalo siyo zuri.

“Hivi karibuni niliposti video nikimshika mchumba wangu kitambi, nilitaka kuwaonesha watu kuwa kitambi siyo shida zangu na hasa wanaume ambao wanahangaika sana kutafuta six-packs.

Rosa Ree amesema kuwa wanaume wanasahau kutafuta pesa mwisho wake ndiyo wanaanza kuitwa vibenten, kwa hiyo kaka zangu, amkeni tafuteni pesa mwanamke atakupenda tu jinsi ulivyo,” anasema Rosa Ree ambaye amechumbiwa hivi karibuni na jamaa aitwaye Petrousse.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *