Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza kuwa pindi atakapotua nchini Tanzania kutoka Marekani ataingia studio kufanya kolabo na msanii mkongwe wa muziki nchini 20 Percent.

Harmonize ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwaajili ya ziara ya kimuziki amesema kuwa kwake ni heshima sana kufanya kazi na mkongwe huyo wa Bongo Fleva.  

Harmonize ameweka wazi hilo kupitia Instastory yake ambayo alikuwa anasikiliza nyimbo za mwanamuziki huyo mahiri wa kuelimisha jamii na kuandika kuwa “Siku nitakayo kanyaga ardhi ya Tanzania hata iwe usiku wa manane nitaenda studio na kaka yangu 20%. Hii ni ndoto yangu”

Endapo Harmonize atakamilisha hilo atakuwa ameendeleza orodha ya wasanii wakongwe ambao amefanikiwa kufanya nao kazi ambapo mpaka sasa ameshafanya kolabo na Lady Jay Dee, Mr Blue na Dully Sykes.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *