Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu amesema kuwa, kipindi cha kukaa uchi ili mtu apate umaarufu kimepitwa na wakati badala yake sasa hivi ni mwendo wa kupiga kazi ili maisha yaendelee.

Amber Lulu anasema kuwa, kwa upande mwingine hata yeye alikuwa akifanya makosa kuacha mwili wake wazi.

Amesema kuwa sasa akili imemkaa sawa na ana mtoto anayemtegemea kwa kila kitu, hivyo hataki kusikia mambo hayo tena kwenye maisha yake.

“Kukaa uchi na kujiachia wazi sehemu kubwa ya mwili kwa sasa ni ushamba na vitu hivyo vimepitwa na wakati kwa sababu hata mimi ninajilaumu sana kwa nini nilifanya hivyo,” anasema Amber Lulu ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Arianna.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *