Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Rosa Ree amewajibu baadhi ya mashabiki wake ambao walishangazwa kuvalishwa pete kwa msanii huyo.

Rosa Ree amewajibu mashabiki zake kwa kusema. “Sasa Hivi Mimi Ni Mchumba Wa King na Nimefurahi Sana Kwasababu Nimetoka Nae Mbali Sana, Tumepanga Mengi Sana Na Tunaomba Mungu Atusaidie Tufanikishe”

“Wapo Ambao Watasema Mimi Bado Ni Mdogo? Lakini Mimi Naamini Kwamba Pale Unapokuwa Na Nguvu Ndio Muda Mzuri Wa Kupanga Future Yako, Kwenye Majukumu Ya Muziki Naamini Muziki Upo Na Utaendelea Kuwepo Napenda Muziki Tangu Nikiwa Mdogo Hadi Sasa Hivyo Hata Nikiwa Mzee Nitaendelea Kuupenda”

“Ukisema Muziki Ufanye Nisifanye Maisha Mengine Haitakua Sawa, Kwaiyo Ukisema Nikifika Miaka 50 Ndio Nianze Kutafuta Mwenza Itakua Uongo Sana, Kifupi Watu Waendelee Kusapoti Muziki Wangu Wajue Pia Sitawaangusha (Kwenye Muziki) Na Naamini Kuna Kitu Wanaweza Kujifunza Kwenye Maisha Yangu”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *