Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imewaonya watu wanaudurufu na kuuza kazi za filamu na muziki ikiwemo albamu mpya ya msanii wa Bongo Fleva Alikiba aliyoiachia hivi karibuni.

Onyo hilo limetolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki, Doreen Sinare kupitia taarifa yake kwa umma.

Albamu hiyo iliyopewa jina la ‘Only One King’  yenye  nyimbo 16, ilizinduliwa wiki moja iliyopita, ambapo inakuwa ni albamu ya tatu kwa Alikiba kuitoa tangu alipoanza muziki.

Hata hivyo juzi kupitia ukurasa wake msanii wa Bongofleva, Baghdadi aliandika kwamba anasikitika kuona albamu hiyo ikiwa inauzwa kama njugu maeneo ya Mwenge.

Hili huenda likawa  limewazindua COSOTA na kutoa tamko hilo la kuonya watu wanaendelelea na kazi za kudurufu kazi za wasanii kuacha mara moja huku akigusia  albamu hiyo ya Alikiba.

Katia taarifa hiyo ilisema “Hivi karibuni baada ya mmiliki wa Rekodi ya Lebo ya Kings Music na msanii wa muziki, Alikiba kutoa taarifa ya kupatikana kwa albamu yake ya ‘Only One King’ katika majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kusambaza kazi za muziki, kumeibuka watu  wanaodurufu kazi hiyo na kuuza mtaani pasipo makubaliano yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *