Mchekeshaji na msanii wa filamu nchini Idriss Sultan ameendelea kukumbushia mpango wake wa kuchukua tuzo ya Oscar huku ambapo ameweka wazi kuwa tuzo hiyo ataichukua kupitia filamu mpya ya Mwalimu.
Idris Sultan amesema hayo wakati wa kuadhimisha miaka 22 toka kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kilichotokea mwaka 1999 nchini Uingereza.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Idriss “MOGUL” ameandika kuwa,”Mnakumbuka ile OSCAR niliyowaaambia nitachukua? Nitaichukua kwenye movie ya Mwalimu.”
Msanii huyo amesema kuwa ameamua kutengeneza filamu kuhusu maisha ya Mwl. Nyerere na mambo aliyofanya akiwa kama Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.