Video za msanii wa muziki nchini Kenya Otile Brown zimerudi YouTube baada ya kuondolewa kwa siku kadhaa bila sababu yoyote lakini sasa zimerudishwa.

Video hizo kwasasa zimerudishwa kwenye mtandao huo kama kawaida huku views wake wakibakia kama ilivyokuwa hapo awali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo amewajuza mashabiki zake kuwa video hizo zimerudi rasmi baada ya kuondolewa YouTube.

Otile Brown ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram”And we’re back on YouTube, asanteni kwa uvumilivu riziki wataichelewesha tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *