Wanamuziki kutoka Jamhuri ya Kongo, Fally Ipupa amesema anafuatilia muziki wa Tanzania kwa karibu na moja ya wasanii anaowakubali ni Barnaba Classic.

Mwanamuziki huyo ameyasema hayo alipotua nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya maonyesho yake katika mikoa miwili ya Dar es Salaam na Mwanza.

Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere pamoja na mambo mengine pia alipata wasaa wa kuzungumza na waandishi wa habari.

Moja ya maswali aliyoulizwa ni kwa namna gani anafuatilia muziki wa Tanzania na ni wasanii gani anawapenda ambapo kati yao alimtaja Barnaba.

Kutokana na kutajwa huko,Mwananchi ilimtafuta Barnaba kujua namna alivyochukulia kutajwa na msanii huyo mwenye tuzo nyingi za muziki za kimataifa ikiwemo MTV Africa na BET.

Katika maelezo yake Barnaba amesema anasikia faraja kwa kuwa wasanii wazuri wapo wengi lakini kutajwa yeye ni heshima kubwa.

“Fally Pupa ni kaka yangu,najisikia faraja kunitaja kuwa moja ya wasanii anaowakubali nami pia namkubali sana kwani huyu ni alama ya muziki wa Afrika, tuna kila sababu ya kujivunia kuwa naye” amesema Barnaba.

Hata hivyo amesema amefahamiana na msanii huyo siku nyingi tangu alipokuja Tanzania miaka kumi iliyopita licha ya kuwa hawajawahi kuimba naye wimbo wa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *