Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa ana wivu kumuona Vanessa Mdee amepata mtoto lakini licha ya hayo yote alimpongeza.
“Im sooo jealous. Congrats my baby,” Wema alimwandikia Vanessa. Kwa upande wake Vanessa alimshauri na kumwambia kwamba wakati wake utafika.
Hata hivyo, kufuatia majibizano hayo kati ya Wema na Vanessa wanamitandao wamemuhurumia na kumtia moyo Wema huku wakisema siku moja Mungu atamshangaza na atakuwa na ushuuda wake.
Mapema mwaka huu, Wema alisema kwamba licha ya kutarajia mengi kutoka kwa mmoja wa wapenzi wake, lakini waliachana kwa sababu hakuwa na uwezo wa kumpa mtoto.
“Kwa kweli nilikuwa nikitarajia kuolewa naye, lakini jambo moja au tuseme moja ya sababu ambazo zilisababisha kuachana kwetu ni kutokuwa na uwezo wa kumpa watoto.
“Ilikuwa mbaya kwangu kwa sababu kama mwanadamu, nilikuwa na matarajio yangu na nilikuwa nikitarajia mapenzi yetu yangechipuka na kuimarishwa na mtoto,” alisema Wema.