Mzazi mwenzie Rayvanny, Fayma maarufu kama Fayvanny amefunguka na kusema kuwa kwasasa hayupo tena kwenye mahusiano na Rayvanny.
Baada ya kuulizwa kuhusu maisha yake na je kwa sasa yupo kwenye mahusiano mengine au yupo single, majibu ya Fahyma yalikuwa kwa sasa nipo kwenye mahusiano.
Fahyma ameeleza kuwa ni kweli alisema Rayvanny hawezi kumuacha kwa sababu yeye ni mtoto wa Kitanga anayajua mapenzi ila alisema kipindi yupo naye.
Fahyma ameeleza kuwa anajutia sana kuhusu maneno aliyomuandikia Rayvanny mtandaoni kuwa yeye ndio anaiharibu familia yake.
Fahyma hakusita kujibu swali kuhusu Rayvanny kwenda kumtambulisha Paula nyumbani kwao Mbeya huku ikielezwa kuwa ndugu zake na Rayvanny walimkataa paula na kumtaka Fhyma.