Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amepanga kuachia kolabo yake nyingine tena akiwa na mkongwe T-Pain kutoka Marekani.
Hali hiyo imekuja baada ya siku chache mwanamuziki huyo kuachi wimbo wake mpya aliomshirikisha mwanamuziki wa Hip Hop nchini Young Lunya.
Maua amerejea akiwa na nguvu mpya baada ya hivi karibuni kutangaza kuwa amepona matatizo yake ya kiafya yaliyokuwa yakimsumbua kwa takribani nusu mwaka na kuwa kimya kimuziki.
Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kwasasa.