Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amezindua rasmi album yake ambayo ameipa jina la THE ONLY ONE KING ambayo itatoka tarehe 7 mwezi wa 10 mwaka huu.
Alikiba ametangaza kuachia albam hiyo baada ya kukamilika rasmi hivyo mashabiki wakae mkao wa kula kuipokea albam hiyo mpya.
Mbali na album Alikiba amefunguka Juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Tour yake nchini marekani lakini amesisitiza mashabiki itakapo anadaliwa basi wajitokeze kwa wingi.
Huku akimaliza kwa kusema yasitokee Kama yaliyotokea kwa wasanii wengine show kushindwa kujaza mashabiki katika uzinduzi wa albam zao.