Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amesema kwamba muziki si kipaumbele chake kwa sasa kwani kazi kubwa aliyonayo sasa ni kuwatumikia wananchi wake kwanza.
Mwana FA ambaye kwasasa ni mbunge wa Muheza mkoani Tanga amesema kuwa kutokana na majukumu yake ya ubunge kuwa mengi hivyo hawezi kuingia studio kwasasa.
Mwana FA amesema kulingana na majukumu aliyonayo inafikia hatua anakosa hata muda wa kufanya mazoezi ili kuweka viungo vya mwili wake sawa.
“Suala la muziki kwa sasa kusema ukweli Mungu atusaidie tutaona namna itakavyokuwa kama tutaweza kufanya tutafanya, lakini ngoja tuwatumikie wananchi wa Muheza kwanza.
Mwanamuziki huyo ametamba na vibao vyake kibao kabla ya kuamua kugeukia masuala ya siasa na kushinda ubunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.