Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amelazimika kufuta na kuahirisha ziara yake ya muziki katika nchi ya Canada na Uswisi ambapo meneja wake amefunguka sababu ya yote hayo.
Harmonize alikuwa amepanga kuwatumbuiza mashabiki wake huko Canada mnamo Oktoba 30, mwaka huu na nchini Sweden, Novemba 6, mwaka huu, lakini ziara yake imeahirishwa.
“Kwanza tunamshukuru Mungu tangu tumefika Marekani tumeshafanya shoo tatu na mapokezi yalikuwa mazuri sana.
“Kwetu sisi tumechukulia kwamba soko letu sasa hivi limekuwa kwa sababu muziki wetu unasikilizwa.
“Naomba niwakumbushe kwamba shoo za Harmonize zimeandaliwa na mapromota na ndiyo wao wanafanya promosheni, lakini hata sisi tunafanya kwa kuwa tumeshafika hapa Marekani,” amesema Mjerumani
“Hali inavyoendelea wanaona labda mkusanyiko wa watu ni hatari hivyo ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wetu kutokana na vizuizi walivyoweka.
“Ni kweli tunatamani sana wasanii wetu wafanye shoo kote huko, lakini ndiyo imekuwa hivyo hawaruhusu mikusanyiko kutokana na ongezeko la wagonjwa.
“Hata hivyo, kwa Ulaya, kama watawahi kufungua na kuruhusu mikusanyiko kwa kuwa tupo huku hadi Desemba tutakwenda kufanya tu bila shida yoyote,” anasema Merumani.
Harmonize au Harmo ambaye ameambatana msanii wake, Ibraah nchini Marekani, wanaendelea na shoo za kimataifa nchini humo.