Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa ataoa mwanamke endapo atakuwa tayari hata kama ndoa yake itadumu kwa wiki moja.

Dully Sykes amefunguka hayo baada ya kushindwa kuoa mwanamke hata mmoja kati ya wanawake 6 tofauti aliopata nao watoto.

“Nitaoa tu, naamini kwenye kuanza watoto kwanza, unaweza kuoa halafu nyumba isifabarikiwe watoto, nitaoa nikiwa tayari, hata kama ndoa yangu itadumu kwa wiki moja ila nitaoa”.

“Mama watoto zangu wote tunalea pamoja na tunashirikiana siyo kwamba natoa mahitaji peke yangu” ameongeza Dully Sykes.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *