Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza kusogeza mbele shows zake ambazo alikuwa anatarajia kuzipiga nchini Canada pamoja na Sweden.
Kwa mujibu wa Harmonize amelazimika kufanya hivyo kutokana na vizuizi vya mikusanyiko kwenye nchi hizo ambazo alitarajiwa kutumbuiza.
Harmonize ameandika “Watu wangu wa Canada na Sweeden ningependa kuwajuza kuwa sitoweza kufanikisha kuja kutumbuiza katika tarehe ambazo zimetangazwa kutokana na vizuizi vinavyotokana na Covid-19.
Kwahiyo nitawataarifu tarehe mpya na kwa wote waliokata tiketi tayari niaminini nitakuja huko kwa mipango ya Mungu”.
Harmonize amemaliza kwa kuwakaribisha waandaaji wa show kuendelea kuwasiliana na kwaajili ya booking za show kwa miji mbalimbali nchini Marekani.
Harmonize alitarajiwa kutumbuiza nchini Canada mnamo October 8,2021 na Sweeden November 6,2021.