Mwanamuziki wa rap Bongo, Rapcha amekanusha taarifa za kupangiwi cha kuzungumza awapo kwenye interviews na bosi wake P-Funk Majani baada uvumi kuenea kuwa kuna baadhi ya vitu hatolei ufafanuzi kutokana na kubanwa koo.
Msanii huyo wa Bongo Records amesema haijawahi tokea akazuiliwa au kupangiwa vitu vya kuzunguma kwani ana amini yeye sio miyeyusho.
“Haiwezi kutokea kitu kama hicho, ujuwe mpaka mtu anakupangia cha kuzungumza basi anajua kuwa huwa unafyatuka ila kwa mtu ambaye ana amini katika msanii wake na anajuwa kuwa hana miyeyusho hawezi kumpangia cha kuzungumza”.
Rapcha ameachia albam hiyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu tu baada ya kuachia ngoma yake ya ‘Lissa’.
Hadi sasa wimbo huo una zaidi ya watazamaji milioni 1.5 kwenye mtandao wa YouTube huku albamu yake mpya ikianza kupatikana kupitia streaming platform namba moja ya muziki barani Afrika, Boomplay.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa albam hiyo, Rapcha ambaye kwa sasa yupo chini ya usimamizi wa ‘Bongo Records’ alisema;
Kupitia albamu hii, nataka mashabiki zangu wamuelewe Rapcha ni nani, kitu ambacho kimenisukuma kutengeneza albam ambayo nina uhakika wa asilimia 100 mashabiki zangu wataipenda”.