Msanii wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Goodluck Gozbert amefunguka kuwa kuna wasanii haongei nao kwasababu ya msimamo wake wa kiimani wa kukataa kuandika nyimbo za kidunia.

Goodluck ameweka wazi hilo kupitia mahojiano yake na kituo cha Redio cha Redio one. Nikimnukuu “Kuna wasanii mpaka sasa siongei nao kwasababu ya misimamo yangu ya kiimani.

Anakufuata anakwambia nataka uniandikie wimbo, unapomueleza msimamo wako wa kiimani inageuka kuwa chuki. Kuna wasanii hawaongei na mimi kwasababu wanahisi nimewanyima kufanikiwa”.

Gooluck ambaye kwa sasa anafanya vizuri kwenye upande wa nyimbo za Injili ni kati ya waandishi bora wa nyimbo za Bongo Fleva na Injili ambapo kwenye upande wa Bongo Fleva ameshawahi kuandika nyimbo mbalimbali kama Moyo mashine ya Ben Poll.

Siachani Nawe ya Baraka The Prince etc ila kwa sasa ameacha kufanya kazi hiyo ya kuandika nyimbo za kidunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *